Tanzania: George Masaju ameteuliwa kuwa Jaji Mkuu

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu.

Bwana Masaju anarithi mikoba ya Profesa Ibrahim Hamis Juma, ambaye alistaafu rasmi baada ya miaka saba katika wadhifa huo.

Mheshimiwa Masaju, aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, aliapishwa Juni 15, 2025, Ikulu ndogo ya Chamwino mjini Dodoma.

Kabla ya uteuzi huu, Mheshimiwa Masaju aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 na mshauri wa masuala ya sheria wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Mapema mwaka huu, aliteuliwa kuwa Tume ya Ardhi, iliyoanzishwa kushughulikia kero za Hifadhi ya Ngorongoro.

Katika hafla ya kuapishwa Rais Samia alitoa shukurani zake kwa Profesa Hamis Ibrahim Juma, aliyekuwa Jaji Mkuu, kwa mchango wake mkubwa wa kuleta mageuzi ya miundombinu, mifumo ya kazi na ufanisi wa Mahakama ya Tanzania, huku akimtaja kuwa kiongozi aliyeacha historia ya kudumu katika utumishi wa taasisi hiyo.

Ikumbukwe kwamba Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imekuwa mwanachama wa CJCA tangu Machi 2015.